Eyal Zamir amemwambia Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu na baraza lake la mawaziri katika mkutano wa hivi karibuni kwamba, "Mikakati ya kijeshi pekee haiwezi kutimiza malengo yote huko Gaza, haswa kwa kukosekana kwa safu ya kidiplomasia."
Utawala wa Israel umetoa wito wa kuteka maeneo mapya ya Gaza. Hata hivyo, wengi wa maafisa wa Israel wameonya kuwa kutekeleza kwa ufanisi hili kunaweza kuchukua muda mrefu sana.
Mamia ya wanajeshi wa akiba wa Israel na maveterani tayari wametia saini maombi ya kutaka kusitishwa kwa vita vya Gaza na kurejeshwa kwa mateka kupitia kubadilishana wafungwa na Hamas. Netanyahu ametishia kuwafuta kazi wanajeshi walioko kazini waliotia saini maombi hayo.
Jeshi la utawala katili wa Israel pia limekuwa likikabiliwa na uhaba wa askari kwa sababu ya kuachiliwa kwa Wayahudi wa Kiothodoxi na kusita na uchovu wa vita wa wanajeshi wa kawaida.
Licha ya mashambulizi yanayoendelea kufanywa na mhimili wa Kizayuni na Marekani dhidi ya Gaza na Yemen, lakini bado vikosi vya jeshi la Yemen na Muqawama wa Palestina vinaendelea kukabiliana na wavamizi hao.
Haya yanajiri siku chache baada ya kundi la askari wa akiba wa jeshi la anga la Israel limefukuzwa kazi baada ya kutia saini waraka wa kutaka kusitishwa vita dhidi ya Gaza na kurejeshwa kwa mateka wa utawala huo haramu.
342/
Your Comment